Usipotenda kwa umakini unaweza kujichukia na mambo mengi hayatoenda sawa. Kila mtu anahitaji mtu mwenye nguvu zaidi yake amnyanyue. Na mtu mwenye nguvu ni yule mwenye busara.
Kwasababu hata kama mtu ana nguvu kiasi gani kama hana busara
atakuja kukamatika tu na asione njia ya kupita. Ni muhimu sana kukaa karibu na
mtu mwenye hekima na kujifunza kutoka kwake.
Matatizo
kila siku yanapiga hodi na yanahitaji hekima kuyatatua. Ni Muhimu sana kuwa na
busara kwasababu ndio yenye kutusaidia kufanya maamuzi yaliyo bora katika
maisha yetu. Itatusaidia kujenga familia zetu na hata taifa letu.
Pesa haiwezi kufanya hivyo. Haiwezi hata kidogo. Bali ukiwa na
pesa na busara umebarikiwa kweli kweli. Jitupe chini na mshukuru Mungu ukiwa na
hivyo vitu viwili vitakupatia Great Comfort. NO man can be Great without
WISDOM. DRINK A CUP OF WISDOM
Kila tendo letu tunalofanya huunda kitu. Hii iwe kwa kujitambua
au kutokujitambua. Lakini wale wanaotenda kwa kujitambua ndio wanaoendelea
zaidi kuliko wale ambao hawatendi kwa kujitambua.
Kushindwa kufanya chaguzi bora ambazo zitakufanya usonge mbele
ni udhaifu wa kiakili. Ndio maana kuna usemi unaosema kabla haujatenda kitu
chochote fikiri kwakuwa huwezi kurudisha muda nyuma ukiisha tenda jambo na
majuto ni mjukuu.
Kwahiyo binadamu anatakiwa kuwa makini katika fikra na matendo
yake. Kutenda yaliyo sahihi na yenye faida sio tu kwake mwenyewe bali pia kwa
jamii yake na taifa lake.
No comments:
Post a Comment