Kwa mujibu wa sheria zetu muda rasmi wa kufanya kazi kama
ulivyowekwa na sheria ni masaa nane yaani kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa
kumi alasiri na muda mwingne kuacha utumike kwa mambo mengine ikiwemo kupumzika
n.k
Sasa chukua simple facts hizi kisha ufanye reflection naamini
kuna kitu utajifunza, siku moja ya kibinaadamu ina masaa 24 lakini sheria zetu
ambazo zimezaa utamaduni zinaelekeza kazi ifanyike kwa masaa 8 ambayo in
fact n asilimia 33 tu ya muda wote kwa siku
Then
wiki moja yenye siku 7 muda wa kazi kwa mujibu wa sheria tena ni siku 5 yaani
jumatatu mpaka ijumaa ambapo kwa dhana ya masaa ni kwamba wiki moja yenye siku
saba mara masaa ishirini na nne unapata kwamba wiki moja ina masaa 168 lakni
muda wa kazi kwa siku tano za wiki kwa masaa nane kila siku n masaa 40 tu kwa
wiki na kuacha masaa mengne 128 kwa mambo mengne nje ya kazi.
Chukua tena simple facts ambazo haziitaji uwe na PhD kung'amua
ni kwamba mwezi mmoja una masaa 720 lkn masaa ya kazi ni 160 tu kwa maana ya
siku 20 za kazi kwa mwezi ,na vivyo hvyo kwa mwaka wenye masaa 8640 muda wa
kazi ni 22% yake yaani masaa 1,920.
Wakati wenzetu wanaanza kujikomboa katika minyororo ya kiuchumi
iwe kwa level ya mtu mmoja mmoja au kwa level ya kitaifa suala la matumizi
sahihi ya muda ilikuaga n kipaumbele chao cha kwanza kwa maana tukiwa na
matumizi sahihi ya muda then yaambatane na utendaji kazi na ufanyaji kazi kwa
bidii na maarifa basi kwa namna yoyote ile lazima tutapiga hatua.
Tatizo na mifumo yetu ni je kwa kuwa muda wa kazi uliopo
kisheria unatupa muda mwingine mwingi wa kufanya mambo mengine sasa hiyo extra
ordinary time tunaitumia productively?? Au ndio muda ambao tunatumia kwa ajili
ya kukifyonza hata kile kilichovuna katika kazi iliyofanyika kwenye yale masaa
8 ya kazi?
Lakini je hata huo muda kidogo wa kazi tunafanya kweli kazi
kizalendo,kwa welendi,juhudi na maarifa? Je tunafanya tukiwa na dhamira ya
kujikomboa kweli?? Au ndio muda huo huo finyu wa kazi tunapachika na mengineyo
nje na utashi na matarajio?
jibu lake ni simple kwamba tunachanganya majukumu katika muda
uliochangamana na kazi na kufanya kazi katika muda uliochangamana na majukumu
matokeo yake tunakosa vipaumbele kwa kuwa hatuna muda mzuri wala uzuri wa muda
hatuujui.
No comments:
Post a Comment