Tunapokubaliana na ukweli kuwa mitandao ya kijamii inarahisisha
upatikanaji wa mapenzi, tukubaliane pia kuwa teknolojia imefanya mwenzi wako
apatikane kiurahisi zaidi.
Tofauti na zamani kwamba ili mtu amfikie mke wa mtu inabidi avae
ujasiri hasa, na kutumia njia za kijasusi ili kumpata, siku hizi urahisi ni
mkubwa. Ukishamjua jina, unamfuata mtandaoni kisha mengine yanaendelea.
Mke
wa mtu ukishapata namba yake ya simu, mambo mengine yanendelea, kuchati na
kupigiana simu. Jamaa anaonesha kumjali mke wa mwenzake kuliko anavyomjali mkewe.
Mwisho mwanamke naye anasaliti. Teknolojia imekuwa kirusi hatari.
Mke wa mtu anapost picha zenye kumuonesha anavyovutia. Mume
hatokei kumsifu mke wake, matokeo yake wakora wanatokeza kumwaga pongezi,
mwisho mwanamke anaona kumbe anapendwa nje kuliko ndani. Matokeo yake anatoa
shukurani zake kwa upendo wa nje.
Mume wa mtu anapita mitanadao ya kijamii anaona warembo wa kila
aina. Anatoa maoni kwenye picha zao au ana-like. Mwingine maoni na like zake
anakwenda kutumbukiza inbox ya mrembo husika. Mrembo akiwa mwepesi naye anajibu
na masuala mengine yanafuata.
Nyumba moja, mume anakuwa ‘bize’ kusifia wanawake wenye
muonekano wa kimitindo, anamwaga pongezi “mtoto ana fugure namba nane”,
mwingine anasifia makalio “mrembo mgongoni amejaliwa”, wakati huo mke wake naye
yupo na picha ya kijana mwanamazoezi “mkaka handsome ana six-pack.” Mume
kumfikia huyo wake wa namba nane ni rahisi, mke naye na kijana wake wa six-pack
anamfikia kirahisi mno. Ni utaratibu huo ambao umekuwa ukisababisha mapenzi na
ndoa viwe kwenye majaribu mazito ya uaminifu. Teknolojia inaziingiza ndoa
nyingi kwenye chumba cha mtihani.
Lipo janga la makundi ya mitandao, mfano WhatsApp na Facebook
Messenger, muunganiko ni mkubwa mno. Unaunganishwa kwenye kundi na watu ambao
ulikuwa hufahamiani nao.
Katika kuchangia mada mbalimbali kwenye kundi, watu wanahama
kutoka kwenye mijadala ya wazi, wanaanzisha mawasiliano ya faragha. Kwamba mtu
ameona namba ya mtu kwenye kundi, anamtumia ujumbe inbox au anampigia simu.
Mawasiliano yanaendelea mwisho wanafikishana kwenye mapenzi.
No comments:
Post a Comment