Haijalishi ukubwa wa harusi uliyofanya kitu cha muhimu ni
unachokwenda kukijenga baada ya harusi, baada ya watu wote kuondoka na kuwaacha
peke yenu mwende nyumbani, mkaanzishe maisha yenu. hiko ndicho cha muhimu na
ndicho kinachotakiwa kupewa umakini mkubwa. Usisahau hilo jua kwamba una kazi
kubwa mbele yako, na usichukulie harusi kwa ukubwa usiostahili zaidi ya kile
unachoenda kukijenga. "Familia"
Harusi
ni ya siku moja, lakini unachokwenda kukijenga huenda kikaishi muda, zaidi ya
uhai wako. Kwakuwa misingi utakayo wajengea watoto wako ndio misingi hiyo hiyo
watakayo wajengea watoto wao. Ubora wa familia yako huenda ukawa pia ubora wa
familia zao.
Inategemea ulivyolelewa na wewe utawalea hivyo hivyo. Kwahiyo
kwa mwanamume hana haja ya kufurahia sana harusi bali kufikiri kazi iliyo mbele
yake. Kulea watoto katika maadili na nidhamu.
Kulea watoto kama simba walio nyikani, ili wakabiliane na
changamoto zote za duniani. Kwasababu maisha ya duniani sio rahisi sana
yanahitaji busara kukabiliana nayo. Unawezaje kufanya harusi kubwa na kujenga
baadae kisicho na thamani? Ewe kichwa cha familia?

No comments:
Post a Comment