Ukiilewa dhana ya dunia halisi tunayoiishi kwa sasa wanadamu
basi itakusaidia kuijua vema nafasi yako kama mwanadamu na namna sahihi ya
kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kuenenda na kasi ya dunia yetu ya sasa.
Kwanza ni vema ukijua ya kwamba tunaishi katika dunia ya kisasa
ambayo inaipa akili nafasi ya kufanya kazi ngumu kwa niaba ya mwili, yaani ni
dunia ambayo kichwa kinatakiwa kifanye kazi ngumu ili kuunusuru mwili.
Ni dunia ambayo dhana ya *Darwin* (survive for the fittest) kwamba ni watu imara tu ndo wenye nafasi ya kuendelea kuwepo inajidhihirisha kwa mapana, kwa sababu ni dunia ambayo makosa yako, shida zako na uzembe wako ni mtaji wa mwingine kuelekea mafanikio yake.
Tupo katika dunia ambayo dhana ya upendo sio tena kitu
kinachokuja kwa asili (naturally) bali ina vichocheo vyake vingi kikubwa kikiwa
ni ziada ya uwezo na utashi binafsi wa mwanadamu husika.
Kuporomoka kwa upendo wa asili miongoni mwa wanadamu kumezaa
dunia ya watu wabinafsi, wenye choyo, chuki na kila aina ya roho mbaya na wenye
kujitazama wao zaidi bila kujali wangap wataumia na kwa kiasi gani kupitia hiyo
mitazamo yao binafsi.
Ni dunia ambayo kuenenda na kasi yake inahitaji akili ya ziada inayochochewa na utashi wa kuyakubali mabadiliko ya kimazingira na kimfumo. sio dunia ya kusubiri furaha kutoka kwa mwanadamu mwenzio, ni dunia ya kuitafuta furaha yako kwa nguvu zako na matarajio yako mwenyewe.
Ni dunia ambayo unaweza hata kufanya biashara na adui wa rafiki
yako kwa maana rafiki wa adui yako sio lazima sana awe rafiki yako, rafiki yako
ni yule tu mwenye kuenenda na fikra na matarajio yako bila kujali matarajio
yako yanawaumiza wangapi na kivipi.
Hamasika.
Nimeona good
ReplyDelete