Kuna watu hufunga safari pamoja mpaka hotelini. Tena wanaweza
kuingia ndani wakiwa wameshikana mikono, kukumbatia na hata kupigana mabusu.
Ajabu ni kuwa wakishamaliza haja zao, kile kichaa chao cha ngono kinawapotea
kwa muda. Wanaona aibu kutoka pamoja, wanaambiana “anza wewe kutoka.” Kichaa
cha ngono hukata mshipa wa aibu.
Mwanaume kwenda kutembea na ndugu wa mkewe au hata mama mkwe
wake, hicho kama siyo kichaa cha ngono ni nini? Mwanamke kutoka na shemeji zake au baba mkwe wake, hicho ni kiwango cha juu kabisa
cha maradhi ya kichaa cha ngono.
Kwa
kawaida kichaa cha ngono hufanya kazi yake iliyodhamiria. Kikikupanda kisha
kikakutuma uwe unatongoza na kutembea na marafiki wa mkeo, hata ukiwa unaumwa
upo kitandani hujigeuzi, wakija kukuona kwa heshima ya urafiki wao na mkeo,
wewe utatumia kila hila mpaka uombe namba ya simu.
Kichaa cha ngono kikimtuma mke wa mtu kuwamaliza marafiki wa
mume wake, atakuwa kimbelembele kuwajali marafiki zake utafikiri mtu kweli.
Ukarimu mwingi, kumbe ule ukarimu wake tafsiri yake ni ngono. Ukishakijua
kichaa cha ngono hakikusumbui.
Usiombe ukutane na mwanamke ambaye anaumwa kichaa cha ngono,
anaweza kuzungukwa na wanaume 10 halafu wote hawajuani, kila mmoja anadhani
yeye peke yake ndiye anakula. Anakuwa na mumewe ambaye anajulikana kisha
marafiki tisa wa mumewe. Hao marafiki kila mmoja anaamini yeye ndiye anakula
kwa siri nje ya mwenye mali. Kumbe wote pale wanakula.
Mwanamke anawapanga, stori za mezani kisha kwenye simu
zinaendelea SMS: “Natamani baada ya kutoka hapa tukalale wote, sema tu jamaa
hapa anabana.” Hiyo SMS anaituma kwa wanaume wote tisa kasoro mume wake, halafu
kila mmoja anaamini katumiwa peke yake, kisha anajibu kwa madaha ya kuamini
anapendwa: “Usijali baby, next time, you know I love you kuliko mume wako.” SMS
hiyo ikajibiwa na wanaume wote tisa, mwanamke huyo roho kwatu kwa kujiona yeye
ndiye mwanamke wa shoka anayeweza kuwaendesha wanaume 10 kwa wakati mmoja bila
kujuana. Anawachanganya tu kama karanga za Saida Kalori. Ile hali ya mwanamke
huyo kujiona mjanja kwa ukahaba anaofanya ndiyo matokeo ya kichaa cha ngono
kukomaa.
No comments:
Post a Comment